Kiwango cha Msingi cha UboranaUwajibikaji cha Kutoa Misaada ya Kibinadamu kinayaelekeza mashirika na watu binafsi namna ya kuhakikisha wanatoa huduma za miitikio ya kibinadamu kiubora, kiufanisi na kiuwajibikaji.
Kiwango cha Msingi cha Kutoa Msaada wa Kibinadamu kina ahadi tisa ambazo zimefafanuliwa katika kozi hii ya mafunzo mtandaoni. Kila ahadii inajumuisha mambo ya msingi na majukumu ya shirika (“kipi unastahi kikutenda”) na viashiria (“Je, unatekeleza ipasavyo?”).
Moduli hii ya mafunzo mtandaoni inatambulisha viwango vya CHS. Hata kama haufanyi kazi na shirika la misaada ya kibinaadamu au hujahusishwa katika utoaji, ni muhimu kila mtu kujua ahadi tisa ambazo zitakusaidia kujua kwa nini mashirika ya kibinadamu yanavyofanya kwa namna mbalimbali.
Kozi imeundwa kwa ushirikiano wa asasi za CHS alliance, Mradi wa Sphere, Gruope URD na IECHAH.
Hadhira
Moduli hii imewalenga watoa huduma ya misaada ya kibinadamu kwa ngazi zote na watu wengine wenye nia na maelezo ya jumla kuhusu CHS
Length
Moduli hii itachukua saa 1-2 kukamilika.
Lugha nyenginezo
Kozi hii pia inapatikana Katika lugha ya Kiingereza, Kifaransa na Kiarabu.