Misingi ya kitaaluma ya programu za mafunzo ya misaada ya kibinadamu, inatoa mtaala kamili unaolenga kujenga uwezo wa kutumia maarifa mapya ili kuwaandaa watoa misaada ya kibinadamu wapya na wale ambao tayari wanafanyakazi katika sekta kwa kuzingatia changamoto watakazokabiliana nazo uwandani.

Programu hii imetayarishwa na kufundishwa na wataalamu kutoka pande zote za dunia, hivyo inajumuisha sifa za kuwa na ustadi wa kitaaluma, usomaji kwa vitendo, mazoezi yanayozingatia ushahidi, malengo ya kujifunza yenye viwango, na majaribio ya kufurahisha na kupima kwa kuzingatia weledi, uchunguzi kifani na majaribio yanayopima utendaji

Programu hii inaundwa na Moduli 4. Kozi hii ina Moduli 2; kwa kusoma zaidi unaweza kupakua katika mitandao ifuatayo hapa chini:

Moduli ya 2: Wapokezi wa misaada ya kibinadamu na Watendaji

Mada katika Moduli

  • Upokezi wa kibinadamu
  • Watendaji wakuu
  • Jeshi
  • Watendaji wa kitaifa
  • Nafasi za kibinadamu

Malengo ya mafunzo:

  • Kufafanua dhana ya upokezi wa kibinadamu
  • Kuorodhesha kategoria tatu za uitikio wa Kibinadamu
  • Kuelezea aina tatu kuu za watendaji wa kibinadamu
  • Kubainisha mashirika yanayojumuisha aina tatu za watendaji wa kibinadamu
  • Kuorodhesha sifa kuu zinazobainisha nafasi ya Kibinadamu

Hadhira

Moduli hii ni mahsusi kwa watendaji wa kibinadamu haswa wale ambao ni wapya katika sekta hii, na wale ambao wenye shauku ya kujiongezea maarifa na wanaojitolea katika mwitikio wa Kibinadamu

Muda

Saa 1

Programu ya Uhitimu ya PHAP: Uelewa wa mfumo wa ecolojia katika kutoa misaada ya kibinadamu. 

Kozi hii itakusaidia kujiandaa na programu ya cheti cha uhitimu cha PHAP katika uelewa wa mfumo wa ecolojia katika kutoa misaada ya kibinadamu (Understanding the Humanitarian Ecosystem).

Kozi inaelekeza haswa sehemu 1.3 na 1.4 ya mwongozo wa tathmini ya uthibitisho. Na pia inaelekeza baadhi ya sehemu ya 2.2

Soma zaidi kuhusu programu ya utoaji wav yeti vya PHAP